Frank Ribery apigwa na shabiki uwanjani.
Na Oscar Oscar Jr
Matukio yameendelea kutokea kila kukicha katika medani ya soka. Ni hivi karibuni tu tulitoka kupata habari za kiungo mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal, Roberto Pires ambaye anacheza soka kwenye ligi kuu nchini India akipigwa makofi na kocha wa timu pinzani.
Ni wiki tu iliyopita, tulipata taarifa za Mbwa kuvamia uwanja na kumng'ata mchezaji kule Brazil na leo, kuna habari za mchezaji wa kimataifa wa Ufaranda na Bayern Munich, Frank Ribery kupigwa uwanjani na shabiki aliyevamia uwanja kwenye mchezo wa kombe la ligi kati ya Hamburg dhidi ya mabingwa hao wa Ujerumani.
Taarifa imeeleza kuwa shabiki mmoja wa timu ya Hamburg alivamia uwanja wakata mchezo kati ya Hamburg dhidi ya Bayern Munich uliendelea hapo jana na kumpiga Frank Ribery na Skafu usoni.
Ribery alikuwa muungwana na hakuweza kujibu kitu chochote kibaya dhidi ya shabiki huyo ambaye baada ya tukio hilo, alitolewa nje na Police huku akitumia vidole vyake kuonyesha ishara ya matusi.
Akizungumza baada ya tukio hilo, Ribery alisema matukio kama hayo ni ya kawaida katika soka na kuongeza kuwa, mashabiki hushikwa na hisia kali. Ribery alifunga bao la tatu kwenye mchezo huo ambao ulimalizika kwa Bayern kushinda mabao 3-1.
Mabao mengine katika mchezo huo, yalifungwa na mshambuliaji Robert Lewandowski na beki David Alaba huku lile la Hamburg likifungwa na Pièrre-Michael Lasogga.
0 comments:
Post a Comment