Danny boy kuwavaa Manchester City
Na Oscar Oscar Jr
Tangu ajiunge na klabu ya Arsenal, mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza Danny Welbeck bado hajacheza hata mchezo mmoja akiwa na timu yake mpya ya Arsenal na Jumamosi hii kuna kila dalili ya kucheza mchezo wake wa kwanza pale Arsenal itakapo umana na Manchester City kwenye dimba la Emirates mchana wa saa 8:45 kwa majira ya Afrika Mashariki.
Welbeck, aliyejiunga na Arsenal akitoka kwa maasimu wao Manchester United kwa ada ya pauni milioni 16 huku muda mwingi akitumika kucheza pembeni na mara chache alitumika kama mshambuliaji kamili wa kati.
Kutokuwepo kwa Olivier Giroud na kiwango duni kilichoonyeshwa na Yaya Sanogo kwenye mechi za hivi karibuni, kuna uwezekano mkubwa Danny Welbeck akaanza kwenye kikosi cha kwanza kitakachovaana na Man City.
Lakini kuna habari mbaya za kuumia kwa mchezaji bora wa timu hiyo wa msimu uliopita, kiungo Aaaron Ramsey ambaye aliumia akiwa anaitumikia timu yake ya taifa ya Wales.
Bado hakuna taarifa zilizothibitika juu ya mchezaji huyo kuwepo au kutokuwepo kuelekea mchezo wao na mabingwa watetezi wa ligi hiyo utaopigwa hapo kesho.
Kuna uwezekano mkubwa Danny Welbeck akafanikiwa sana akiwa na Arsenal kama kocha Wenger atamuamini na kumpa nafasi ya kutosha.
Welbeck ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kufunga, ananguvu na ni aina ya mchezaji anayejua namna ya kujipanga hasa kwenye mashambulizi ya kustukiza na hivi karibuni ametoka kufunga mabao mawili akiwa na timu yake ya taifa ya Uingereza.
0 comments:
Post a Comment