Searching...
Image and video hosting by TinyPic
5 August 2014
Tuesday, August 05, 2014

Yaweza kuwa mwisho wa The special one?


Na Abuu Hozza
 0759422148 

Pamoja na ujeuri wake bado Jose Mourinho ni kama mfalme pale katika viunga vya dimba la Stamford Bridge, historia ya mafanikio yake ya muda mfupi ndani ya club hiyo kwenye awamu yake ya kwanza hayawezi kupuuzwa hata na mtu ambaye sio shabiki wa Chelsea.

Ameipa mafanikio klabu hiyo katika kipindi kifupi ambacho ameweza kudumu na watoto hao wa darajani chini ya uangalizi imara wa mmiliki mrusi Roman Abromovich.

Mourinho wa sasa hawezi kufananishwa na yule wa 2004 mpaka 2007, kipindi hiki tayari ameonekana kuonja ladha ya kufeli. Msimu wa 2012/13 akiwa na kikosi bora cha Real Madrid alitoka kapa. Amerudi tena darajani lakini pamoja  na nguvu ya pesa za mrusi bado ametoka tena patupu.

Yaweza kuwa huu ni mwisho wa The Special One? Mourinho huyu amepoteza ushawishi wake wa kushinda kwa kiwango kikubwa, katika hali ya sasa anaweza kuwa sio yule shujaa wa zamani tena wa Chelsea muda pekee ndio utaongea.

Unajua ni kwanini Mourinho anauza wachezaji nyota wa Chelsea kwa fujo? ni kwa sababu anaamini yeye ndio mtu pekee wa kuabudiwa kuliko mwingine yoyote.

Atafanya kila njia athibitishe mamlaka yake kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na hasa kwa wachezaji wake. Wakati msimu wa 2012/13 mashabiki wa Chelsea wakiamini watashinda taji la ligi kuu ya England kwa ubora wa Juan Mata , Mourinho aliamini ni Oscar pekee ndio mtu sahihi wa kumpa taji.

Wakati mashabiki wakiamini kwamba msimu huu kinda Romelu Lukaku atakuwa ameiva, yeye kumuuza na kumrudisha babu Didier Drogba!

Mashabiki wa Chelsea wanajisahau na kumuona Mourinho ni kama mungu wao. Mourinho anatamani kwenye timu yake kila mchezaji awe kiungo mkabaji au beki. Juan Mata na Kevin de Bryune waligeuka wahanga wake kwa kigezo tu cha kuwa hawawezi kurudi nyuma kukaba.

Nini kinampa jeuri Mourinho kuuza wachezaji anavyotaka yeye? Chelsea fc ni zaidi ya Mourinho, alikuja na akaondoka baadaye kwenda Inter lakini mafanikio yalifuatia bila hata yeye kuwepo.

Timu ilishinda kombe la vilabu bingwa Ulaya chini ya Di Matteo, ikashinda Premier League na FA chini ya Carlo Ancelotti, Europe league chini ya Rafael Benitez. 

Abromovich alitamani kuiona Chelsea inayocheza mpira wa kuvutia, aliwekeza kwa kununua wachezaji mafundi akiamini watakidhi matamanio ingawa baada ya mwamba kurudi amewageuza tena mafundi kama kina Hazard kucheza mpira kama wa West Ham au Stoke City! 

Chelsea imekuwa ikicheza vile anavyotaka yeye akilala akiamua kesho apaki basi bado mashabiki wa Chelsea watamuona bora.Utatu mtakatifu wa Mata,Hazard na Oscar anagalau uliwafanya wasiopenda Chelsea wakose sababu ya kuwachukia, lakini kwa jose haukudumu hata miezi mitatu ukapotea. 

Mourinho ni lazima ajue kuwa watu wanalipa pesa zao kwenda kutazama burudani na wala sio kuona umaridadi wa kukaba.
Ni ngumu kutabiri tena nini kitajiri katika ndoa hii ya pili kati ya Mourinho na Chelsea lakini wakati haudanganyi. 

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!