Na Oscar Oscar Jr
Mechi ya kwanza ya ligi kuu ya Uingereza ilishuhudia wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani wanaoitumikia klabu ya Arsenal wote wakipumzisha lisha ya kuwa wamesharipoti kwenye klabu.
Wenger hakuona kama kuna sababu ya msingi ya kuwatumia mapema kwani kikosi cha kwa sasa ni kipana zaidi.
Kutokana na muda mfupi wa kupumzika walionao Gunners na uchovu wa mechi yao ya kwanza na Majeruhi ya Kieran Gibbs aliyepatwa na jeraha la misuli na Jack Wilshere kugongwa kwenye mchezo huo, Mfaransa huyo alikiri kwamba anashawishika sana kuwaita Wajerumani hao.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kwamba anadhamiria kuwaita wachezaji wake wa Ujerumani walioshinda Kombe la Dunia warudi kwenye kikosi mapema kwa ajili ya mechi ya kwanza ya kufuzu kwa makundi katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumanne ugenini Besiktas.
Gunners wataenda Uturuki baada ya kutolewa jasho mechi yao ya kwanza Ligi ya Premia nyumbani dhidi ya Crystal Palace ambao hawakuwa na meneja, na ambapo waliokolewa na bao la dakika za mwisho kutoka kwa Aaron Ramsey lililowawezesha kushinda 2-1 dhidi ya vijana 10 wa palace.
Wenger alikuwa amewapa Wajerumani wake Mesut Ozil, Per Mertesacker na Lukas Podolski muda zaidi wa kupumzika baada ya taifa lao kushinda Kombe la Dunia Brazil mwezi jana
.
0 comments:
Post a Comment