Mourinho atangaza kupanga mziki mnene vs Burnley
Na Oscar Oscar Jr
Baada ya kumaliza kwenye nafasi ya tatu msimu uliopita, vijana wa Jose Mourinho timu ya Chelsea kesho watajimwaga dimbani kuwakabili Burnley ugenini ambao wamepanda daraja.
Burnley tayari wameongeza wachezaji wapya wanane kwenye kikosi chao na jumatatu usiku wanataka kuwashangaza Chelsea.
Jose Mourinho atakuwa na mtihani mkubwa ugenini juu ya uteuzi wa kikosi cha kwanza na tayari amesema kuwa atateuwa kikosi kamili cha nguvu ambacho kinadaiwa kuwajumuisha Cecs Fabrigas aliyejiunga akitokea klabu ya Barcelona na mshambuliaji Diego Costa aliyetokea Atletico Madrid.
Mtihani pekee utakuwa golini ambapo Mourinho hajabainisha kama atakuwa ni Peter Cech au Thibaut Courtois.
Burley mara ya mwisho kushiriki ligi kuu ilikuwa msimu wa 2009/2010 na katika mchezo wao wa kwanza nyumbani wa msimu huo, waliibuka na ushindi dhidi ya Manchester United na kuwashangaza wengi.
Burnley watakuwa na mshambuliaji wao hatari aliyefunga mabao 21 wakiwa Championship Danny Ings na kesho anatarajiwa kuanza na Jutkiewicz kwenye safu ya ushambuliaji.
Msimu uliopita tulishuhudia timu iliyopanda daraja ya Cardiff City ikimfunga Manchester City kwa hiyo, Jose Mourinho na vijana wake wanatakiwa kuwavaa Burnley kwa tahadhari ya hali ya juu.
0 comments:
Post a Comment