Searching...
Image and video hosting by TinyPic
18 August 2014
Monday, August 18, 2014

Liverpool kuingia sokoni kumnasa mshambuliaji



 Na Oscar Oscar Jr

Licha ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Southampton, kocha wa Liverpool bado anaonekana kutokuwa na imani na safu yake ya ushambuliaji na amepania kuhakikisha kuwa anasajili mtu wa kazi kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Brendan Rodgers aliwaanzisha Sturridge na Sterling kwenye safu ya mashambulizi, na mchezaji mpya, fowadi wa Uingereza Rickie Lambert, akiwa kwenye benchi dhidi ya timu yake ya awali. 
 
Meneja huyo wa Liverpool alimmwagia sifa Sturridge, aliyefunga mabao 21 ya ligi msimu uliopita na aliyefangia bao la ushindi dakika ya 79. 

Liverpool ilimpoteza mshambuliaji wake matata Luis Suarez ambaye alifunga mabao 31 msimu uliopita na kwa sasa ametimkia kwenye klabu ya Barcelona ya Hispania. 

Ni vigumu kumpata Suarez mwingine lakini wapo wachezaji wengi tu wanaoweza kuisaidia safu ya ushambuliaji ya Liverpool akiwemo Radamel Falcao ambaye anatajwa kuwindwa na majogoo hao wa jiji la Liverpool.

Bao la Sturridge kwenye mchezo wao dhidi ya Southampton lilikuwa la 36 katika mechi 50 ambazo ameitumikia timu ya Liverpool tangu alipojiunga misimu miwili iliyopita akitokea klabu ya Chelsea.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!