Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 August 2014
Friday, August 01, 2014

Stand United ni kama Mbeya City.

Na Oscar Oscar Jr


Ligi kuu Tanzania bara ya msimu wa 2014/2015 inatarajia kuanza septemba 20, 2014 huku kukiwa na timu tatu zilizopanda daraja ambazo ni Stand United ya mkoani Shinyanga, Ndanda Fc ya Mtwara na Polis Morogoro ya mkoani Morogoro ambazo zitafikisha jumla ya timu 14 zitakazochuana msimu ujao.

Mbeya City ya mkoani mbeya ni moja kati ya timu zilizoleta changamoto kubwa sana msimu uliopita huku ikiwa timu ngeni baada ya kupanda daraja kwa mara ya kwanza msimu wa 2012/2013. Moja ya mafanikio ya Mbeya City ni kulimaliza kwenye nafasi ya tatu huku ikiwa na alama 49, ikifunga mabao 32 na kuruhusu mabao 19 tu kutikisa nyavu zao. Mbeya City walizunguka kila mkoa na mashabiki wao na kitu pekee kinachowapa dosari ni vurugu na fujo za mara kwa mara ambazo mashabiki wao wamekuwa chanzo.

Stand United ambayo itashiriki ligi kuu msimu ujao, tayari imekuwa gumzo kutokana na kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa na wadau wa soka wa kanda ya ziwa lakini, nao wanaonekana kuanza vurugu mapema kabisa kwenye michezo tu ya kirafiki.

Mashabiki wa timu hiyo wanaonekana kutokubalina na maamuzi ya waamuzi na hili limejidhihirisha kwenye mchezo wao dhidi ya Ambassador ya Kahama uliomalizika bila kufungana. Mashabiki wa United waliosafiri na timu hiyo ya mkoani Shinyanga walianzisha fujo kitu ambacho kililazimu Askari Polis  kuingilia kati.

Watu wa kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla ni lazima waelewe kuwa mchezo wa soka ni mchezo wa watu wastaarabu, kufanya vurugu za aina yoyote uwanjani haifanya matokeo yabadilike. Watu wa Shinyanga na wapenzi wa soka ni lazima wawe watu wanaokubali matokeo. Kuna mambo mengi yakujifunza kupitia Mbeya City lakini sio vurugu na fujo.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!