Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 August 2014
Friday, August 01, 2014

Simba mpya inaendelea kujengwa.

Na Oscar Oscar Jr


Moja kati ya maeneo yaliyoonekana kupwaya kwenye kikosi cha simba msimu uliopita ni safu ya kiungo hasa kiungo mkabaji. Mara kadhaa simba walionekana kumtumia Said Ndemla na Jonas Mkude na pale Mkude alipokuwa nje kwa majeruhi, Amri Kiemba alilazimika kwa nyakati tofauti kurudi chini na kusaidia safu hiyo kitu ambacho hakikuweza kuisaidia sana timu ya Simba.

Simba wameonekana kuanza kulifanyia kazi eneo hilo na wameanza kwa kumsajili kiungo aliyekuwa anakipiga na klabu ya Mtibwa Sugar, Shabani Kisiga na sasa kuna habari za kumleta kiungo mwingine raia wa Burundi, Pierre Kwizera. 

Tatizo kubwa la timu ya Simba linaonekana ni kukosa kiungo mkabaji wa kusaidiana na Mkude na mara kadhaa Simba ilipomkosa kiungo huyo, ilionekana kukosa mtu wa kuziba nafasi yake.

Pamoja na kuwa na safu nzuri ya ushambuliaji ambayo ilifunga mabao 41 msimu uliopita huku Amisi Tambwe akiibuka mfungaji bora baada ya kufunga mabao 19, wekundu wa msimbazi wapo kwenye harakati za kuongeza washambuliaji wengine. 

Paul Kiongera kutoka klabu ya KCB ya nchini Kenya na Jerome Rama raia wa Botswana anayekipiga kwenye klabu ya TP Mazembe naye anatajwa kutua Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Kama Simba watafanikiwa kumnasa Jerome ambaye mpaka sasa amecheza mechi 37 akiwa na timu yake ya taifa ya Botswana huku akifunga mabao 20 na Mshambuliaji Kiongera raia wa Kenya, ni wazi kuwa safu ya ushambuliaji pia itakuwa imeimarika. 

Simba pia imeshakamilisha usajili wa mlinda mlango Hussein Sharrif kutoka Mtibwa sugar ambaye atakuwa na kazi ya kugombea namba na kipa namabari moja Ivo Mapunda.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!