Delay Blind kuiokoa Man United?
Na Oscar Oscar Jr
Bado mambo si mambo kwa wababe wa Manchester United baada ya kuendelea kupata matokeo yake ya kusua sua huku presha kubwa ikiwa kwenye dirisha la usajili. Tayari United wamepata sare mbili na kupoteza mchezo mmoja katika mechi tatu za awali za ligi kuu.
Mashabiki wa Man United kwa sasa wanashangilia zaidi kila usajili wanaoufanya kuliko matokeo yao uwanjani. Kila mchezaji anayesajiliwa na timu hiyo anachukuliwa kama mkombozi kitu ambacho kina wafanya waishi kwa presha muda wote.
United bado inatatizo kwenye safu yake ya Kiungo mkabaji na safu ya ulinzi na tayari taarifa za usajili wa beki wa Uholanzi Daley Blind zinachukuliwa kama njia moja ya kuimarisha kikosi hicho.
Beki huyo amesema anajivunia sana kujiunga na Manchester United baada ya mkataba wake wa pauni 13.85 milioni wa kuhamia huko kutoka Ajax Amsterdam kukamilishwa Jumamosi.
Ndiye Mholanzi wa tisa kujiunga na United akifuata nyayo za Arnold Muhren, Raimond van der Gouw, Jordi Cruyff, Jaap Stam, Ruud van Nistelrooy, Edwin van der Sar, Alexander Buttner na Robin van Persie.
Pamoja na watu wengi kulitazama tatizo la beki na kiungo kama chanzo cha timu hiyo kuporomoka, safu ya ushambuliaji nayo imekosa watu makini wa kutengeneza nafasi za kufunga.
Ashley Young na Vallencia bado hawaonekani kutimiza majukumu yao na pengine ujio wa Di Maria unaweza kutatua tatizo hilo.
0 comments:
Post a Comment