Luiz Suarez ndani ya kikosi cha Barcelona
Na Oscar Oscar Jr
Mshambuliaji wa Uruguay Luiz Suarez, ambaye hataweza kuchezea Barca mechi ya ushindani hadi Oktoba baada ya rufaa yake ya kufungiwa miezi minne kutokana na kumng’ata difenda wa Italia Giorgio Chiellini wakati wa Kombe la Dunia jana alipata nafasi ya kukipiga na Barcelona kwenye mchezo wa kirafiki.
Luis Suarez alichezea Barcelona mechi yake ya kwanza baada ya kuhamia huko kutoka Liverpool kwa €95 milioni huku klabu hiyo ya Catalunia ikikomoa Club Leon ya Mexico 6-0 mechi ya kirafiki Jumatatu.
Barca walikuwa tayari wanaongoza 4-0 kutokana na mabao ya Lionel Messi, Munir El Haddadi na mawili kutoka kwa Neymar kabla ya Munir na Sandro kukamilisha ufungaji mabao yao.
Licha ya utata unaozingira historia yake, ambao ni pamoja na kuwahi kufungiwa mara mbili awali kwa kuuma wachezaji pamoja na kusimamishwa kucheza na Shirikisho la Soka la Uingereza kwa kumtusi kwa ubaguzi wa rangi difenda wa Manchester United Patrice Evra, Suarez alikaribishwa vyema na mashabiki wa nyumbani alipoingia uwanjani.
Messi alifunga la kwanza kwa kichwa dakika tatu kutoka kwa krosi ya Neymar iliyokuwa imepinduliwa.
Straika huyo wa Brazil baadaye aliongeza la pili kwa ustadi baada ya kupokea mpira kutoka kwa Andres Iniesta kabla ya kujifungia lake la pili usiku huo kwa kisigino kwenye wavu wazi dakika mbili kabla ya muda wa mapumziko.
Munir aliingia badala ya Neymar wakati wa mapumziko na akafunga la nne pale Dani Alves alipogonga mpira kutoka kwa Ivan Rakitic na ukaanguka katika njia ya mchezaji huyo wa miaka 19.
Na muda mfupi baada ya Suarez kuingia, Munir alifunga lake la pili kwa kombora zito la chini na kukamilisha uchezaji mzuri wa Barca dakika moja kabla ya mechi kumalizika.
0 comments:
Post a Comment