Searching...
Image and video hosting by TinyPic
19 August 2014
Tuesday, August 19, 2014

Fabregas aing'arisha Chelsea ugenini



Na Oscar Oscar Jr
 
Baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1, Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alisema anatumai kipa Petr Cech atasalia katika klabu hiyo licha ya kupoteza nafasi yake ya kuanza mechi kwa Mbelgiji Thibaut Courtois. 

Courtois, 22, aliyerudi Chelsea baada ya kufanya vizuri akiwa na Atletico Madrid kwa mkopo, alitumiwa na Mourinho mechi ya kwanza ya Ligi ya Premia Jumatatu, waliyoshinda 3-1 ugenini Burnley. 

Cech amekuwa kipa nambari wani wa Chelsea tangu ajiunge na klabu hiyo miaka 10 iliyopita, na alikuwa kwenye vikosi vilivyoshinda Ligi ya Premia mara tatu na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2012. 

Chelsea walionekana kucheza vizuri dakika 45 za kipindi cha kwanza huku Cesc Fabregas aliyejiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Barcelona akionyesha ufundi wa hali ya juu na kutengeneza bao moja maridadi lililofungwa na mjerumani Andre Schurrle.

Mourinho alifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwatoa Oscar, Eden Hazard na Andre Schurrle huku wakiingia mkongwe Didier Drogba, Willian na Obi Mikel na kufanya mchezo upungue kasi na dalili za kupaki bus zilianza kuonekana.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!