Na Oscar Oscar
1. Nawapa nafasi Arsenal, Man United na Chelsea ya kutwaa ubingwa wa EPL msimu huu unaoanza leo. Vijana wa Arsenal wamekaa pamoja kwa muda mrefu sasa na usajili uliofanywa utaongeza nguvu huku kukiwa na uwezekano wa Alexies Sanchez kubadilishwa na kucheza kama striker.
Chelsea, wamefanya usajili mzuri na kukifanya kikosi kuwa na ubora unaolingana karibu kwenye kila nafasi kati ya mchezaji anayeanza na yule anayetokea benchi.
Huu ni muda wa Chris Smalling na Phl Jones kung'aa na kuithibitishia dunia vipaji vyao. Uwepo wa Loius Van Gaal umefanya nidhamu irejee, Kukosa Uefa kutawapa nafasi ya kujikita kwenye ligi tu. Unahodha wa Rooney na uwepo wa fungu la usajili unampa fursa kocha ya kumsajili mchezaji yoyote. United wanaitafuta top four na ubingwa pia.
2. Nimewaondoa Man City kwa sababu kuu tatu, wachezaji wake wametumia sana nguvu misimu mitatu iliyopita na kutwaa taji mara mbili, hawa ni watu kuna kuchoka na kuridhika.
Pili, bado hakuna mbadala wa Yaya Toure na Kompany na mwisho, wachezaji hupigana sana hasa mikataba yao inapoelekea mwisho ili kutengeneza mazingira ya kupata donge nono, wachezaji wengi wa Man City wameshalifanya hilo na wengi wametoka kusaini hivi karibuni.
3. Liverpool, nimewaondoa pia kwenye mbio za ubingwa kwa sababu tatu, moja ni namna walivyotumia nguvu sana msimu uliopita kitu kinachonifanya nione baaadhi ya wachezaji watakuwa na uchovu, pili ni kutosajili kiungo mkabaji "World class" ili Gerrard apate muda wa kupumzika na
Tatu, watalazimika kucheza weekend na katikati ya wiki Uefa kitu ambacho kama watafika mbali kwenye Uefa, kitapunguza nguvu yao kwenye ligi kuu.
Spurs na Everton, nasubiri wani surprise.
0 comments:
Post a Comment