Searching...
Image and video hosting by TinyPic
18 August 2014
Monday, August 18, 2014

Jumanne hii Real Madrid vs Atletico Madrid



Na Oscar Oscar Jr

Baada ya kuchezea kichapo cha bao 4-1 kwenye fainali ya klabu bingwa ulaya, Atletico Madrid kesho watakutana uso kwa uso na wababe wa Ulaya timu ya Real Madrid kwenye mchezo utakaoashiria kufunguliwa pazia la ligi kuu ya Hispania.

Pamoja na kuwapoteza nyota wake muhimu kama Filipe Luiz, Thibaut Courtois na Diego Costa waliojiunga na klabu ya Chelsea huku David Villa akitimkia Marekani, tayari kocha Diego Simione amewanasa Antonie Greizman, Mario Mandzukic na Raul Jimenez na hivyo kuendelea kuimarisha chama lake.

Kwa upande wa Real Madrid wao walifanikiwa kumnasa mfungaji bora wa michuano ya kombe la dunia James Rodriguez, Ton Kroos na golikipa Keylor Navas ambaye bado hajaapata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kocha Carlo Anceloti kutokana na Iker Cassilas kuendelea kuwa chaguo la kwanza.

Real Madrid walianza vizuri kwenye ufunguzi wa pazia la ligi ya Mabingwa Ulaya pale walipowalaza Sevilla kwa bao 2-0 huku mchezaji bora wa dunia Christiano Ronaldo akifunga mabao yote na kuwafanya watoto wa Bernabeu kuibuka na taji lao la kwanza kwa msimu huu.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!