TIMU YA YANGA IKO FIT KUPAMBANA NA JKT OLJORO HAPO KESHO
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young Africans kesho watashuka dimbani kusaka pointi 3 muhimu kwa kucheza na timu ya JKT Oljoro mchezo utakaofanyika kwenye dimba la Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Kikosi cha Young Africans kiliwasili jana jioni jijini Arusha na kufikia katika hotel ya Joshmal eneo la stand na leo asubuhi wachezaji wamefanya mazoezi kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambao ndio utakaotumika kwa mechi kesho.
Kocha Mkuu wa Young Africans Hans van der Puijm amesema anashukuru vijana wake wako salama, wachezaji wote 23 waliopo kambini jijini Arusha wako fit kwa kuajili ya kusaka pointi 3 muhimu ambazo zitaisogeza kwenye nafasi nzuri ya kutetea Ubingwa.
Young Africans inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom ikiwa na pointi 52 nyuma ya Azam FC yenye pointi 55 huku timu zote zikiwa zimebakisha michezo miwili kabla ya kumalizika kwa ligi.
Wachezaji waliopo kambini jijini Arusha ni:
Walinda milango: Deogratias Munish "Dida" na Ally Mustafa "Barthez"
Walinzi: Juma Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Amos Abel, Rajab Zahir, Ibrahim Job, Kelvin Yondani na Nadir Haroub "Cannavaro".
Viungo: Hamis Thabit, Nizar Khalfani, Frank Domayo, Hassan Dilunga, Salum Telela na Sospter Maiga
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Hamis Kizza, Jerson Tegete, Mrisho Ngasa, Saimon Msuva, Said Bahanuzi na Hussein Javu
Taaifa hii ni kwa mujibu wa website ya yanga.
0 comments:
Post a Comment