Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 April 2014
Sunday, April 13, 2014

CHELSEA WAMESHINDA BAO 1-0 DHIDI YA SWANSEA


 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Chelsea wanaoshikilia nafasi ya pili kwenye ligi walishinda 1-0 ugenini dhidi ya Swansea City Jumapili, wakitumia vyema nafuu ya kucheza dhidi ya wachezaji 10 sehemu kubwa ya mechi. Kwa ushindi huo, wameendelea kuwekea presha kwa viongozi wa Ligi ya Premia Liverpool. 

Chelsea sasa wako alama mbili nyuma ya Liverpool baada ya kucheza mechi 34 kila timu na timu hiyo ya Jose Mourinho itazuru Anfield kwa mechi ambayo huenda ikaamua mshindi wa taji katika kipindi cha wiki mbili. 

Awali, klabu hiyo ya Merseyside ilijiimarishia matumaini ya kushinda taji la kwanza la Uingereza katika miaka 24 kwa ushindi wa kusisimua wa 3-2 dhidi ya Manchester City walio nambari tatu na ambao sasa wako alama saba nyuma ya viongozi hao ingawa wana mechi mbili hawajacheza. 

Chelsea walidhibiti mechi baada ya difenda wa Swansea kutoka Uhispania Chico Flores kufukuzwa uwanjani kwa kadi nyekundu robo ya kwanza ya saa baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano. 

Lakini walishindwa kufunga hadi bahati ilipowaangukia dakika ya 67 pale Demba Ba, shujaa wao wa ufungaji mabao wakati wa ushindi wao robofainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Paris Saint-Germain Jumanne, kuwafanyia mambo tena. 

Swansea, ambao wameshuka hadi kwenye klabu sita za mwisho tangu kufukuzwa kwa meneja wao Michael Laudrup februari, sasa wako alama tatu pekee juu ya eneo la kushushwa daraja, wakiwa wamesalia na mechi nne pekee za kucheza.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!