Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 April 2014
Sunday, April 13, 2014

SASA BRENDAN RODGERS AMEANZA MAJIGAMBO



Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Meneja Liverpool Brendan Rodgers alisifu uchezaji wa “kipekee” ulioonyeshwa na timu hiyo na kuiwezesha kupiga hatua kuu katika kukaribia taji la kwanza la Ligi ya Premia kwa ushindi wa kusisimua wa 3-2 nyumbani dhidi ya Manchester City Jumapili. 

Ushindi huo wa 10 mfululizo wa Liverpool uliwafikisha hadi alama 77, alama mbili mbele ya Chelsea – ambao walicheza dhidi ya Swansea mechi ya kuchelewa Jumapili na kushinda bao 1-0– na muhimu sana, alama saba mbele ya City ambao wana mechi mbili hawajacheza wakilinganishwa na timu hiyo ya Merseyside. 

Liverpool wamesalia na mechi nne za kucheza na wakishinda zote, basi watakuwa wametwaa taji kwa mara ya kwanza katika miaka 24.
“Ulikuwa uchezaji wa kipekee,” Rodgers aliambia Sky Sports.
"Ninadhani tulikuwa na siku ya kipekee sana leo. Ninafikiri ulimwengu uliokuwa ukitazama uliona timu yenye moyo, na ustadi.” 

Kama walivyofanya mara nyingi sana msimu huu, Liverpool walianza mchezo kwa kasi na kupata uongozi dakika ya sita Raheem Sterling alipowabwaga Vincent Kompany na Joe Hart na kisha kufunga. 

Martin Skrtel baadaye alifunga bao lake la saba msimu huu dakika ya 26 na kuongeza uongozi wao.
City walijibu kwa magoli mawili katika dakika tano kutoka kwa David Silva dakika ya 57 na bao la kujifunga la Glen Johnson na kufanya mechi kuwa ya kusisimua sana. 

Huku sare ya nne ya 2-2 kwenye mechi tano sasa kati ya timu hizo mbili yakionekana karibu sana, Philippe Coutinho alitumia vyema kosa la Kompany la kutoondoa mpira vyema eneo la hatari na kuwahakikishia ushindi. 

"Tulidhibiti kabisa mechi. Muda wa mapumziko tulikuwa 2-0 mbele na hata mabao yangekuwa mengi,” Rodgers akaongeza.
"Hongera kwa Man City kwa sababu tukiwa 2-0 tulikuwa hatushikiki kipindi cha kwanza. Unatarajia kuwe na dakika 15-20 zao kurejea kwenye mechi. 

“Wao (wachezaji wa Liverpool) walionyesha sifa nzuri tulizo nazo katika kundi hili – kujikusanya tena na kufunga bao safi sana na kutwaa alama tatu muhimu sana.”


Klabu hiyo ilitoa heshima stahiki wikendi hii ya ukumbusho wa miaka 25 tangu kutokea kwa mkasa wa Hillsborough ambapo mashabiki 96 wa Liverpool walifariki wakati wa mechi ya Kombe la FA dhidi ya Nottingham Forest, na Rodgers alikiri kwamba klabu yake ilitumia ukumbusho huo kujipa motisha. 

"Huwa daima kuna timu yenye hisia nyingi hasa kipindi kama hiki. Tukienda kwenye mechi hiyo, mengi yalisemwa kuhusu kama hayo yangeathiri wachezaji. Huwa twaishi nayo kila siku.
“Familia na walioathiriwa wa Hillsborough huwa nasi kila siku. Lilikuwa ni jambo la kutupa motisha badala ya kuturudisha nyuma.” 

Athari za hafla hiyo na mechi ya kusisimua iliyochezwa kwa kasi sana zilionekana wazi. Nahodha wa Steven Gerrard alitokwa na machozi baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa, na hisia zake zilionekana wazi wakati wa mahojiano ya baada ya mechi. 

"Huwa natekwa na hisia lakini tunahitaji kutulia,” akasema. “Bado tuna mechi nne kuu zilizobaki lakini hilo lilikuwa na maana kubwa sana kwetu, hasa waliporudi kwenye mechi. Huwa unahofia mabaya kutokea wakati kama huo. 

“Hizo ndizo siku 90 ndefu zaidi ambazo labda nishawahi kucheza. Nilihisi kana kwamba mshale wa saa ulikuwa unarudi nyuma badala ya kusonga mbele baadhi ya sehemu za mechi hiyo.
"Tunataka kwenda hadi mwisho. Hatujashinda chochote kwa sasa lakini huu ndio labda ujumbe mkuu ambao tumetoa kufikia sasa.”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!