Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 April 2014
Friday, April 04, 2014

KUN AGUERO AMEREJEA NA ATAKUWA FITI DHIDI YA LIVERPOOL

 

 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Mshabuliaji hatari wa klabu ya Manchester CitY, Sergio Aguero hawezi kuwa tayari kuelekea mchezo wa jumamosi dhidi ya Southampton, lakini kocha Manuel Pellegrini amethibitisha kuwa,atapatikana kwenye mechi zao kuanzia wiki ijayo kuelekea mchezo wao dhidi ya Liverpool. 

Aguero ambaye tayari anamagoli  15 kwenye mechi 17 za ligi msimu huu,hajacheza tena mechi yoyote tangu alipopata maumivu kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa kule Camp Nou dhidi ya Barcelona mwezi uliopita.

Wakiwa na alama 67 na kusalia nafasi ya pili, alama nne pungufu kwa vinara Liverpool na mbili dhidi ya waliopo nafasi ya pili timu ya Chelsea bado,wana mechi mbili mkononi dhidi ya aliyeko nafasi ya kwanza na ya pili.

Kurudi dimbani kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25-itakuwa ni msaada sana kuelekea mechi yao na watoto wa Merseyside Liverpool,hii ni mechi ambayo inamtazamo wa kuamua bingwa wa ligi kuu msimu huu.

" nadhani mechi hii (Southampton) itakuwa ni mapema sana kwa Sergio," Pellegrini amewaambia wanahabari siku ya ijumaa.
"Amefanya mazoezi kwa siku mbili tu na nadhani anahitaji muda zaidi.Labda wiki moja au zaidi ili awe fiti kwa ajili ya mechi yetu na   Liverpool.

"Tuna amini atakuja kutoa mchango mkubwa kwenye mechi zetu zilizosalia lakini,kwa mechi ya Southampton bado nimapema sana kuanza kumtumia.Anahitaji mapumziko zaidi ili awe amepona kwa aislimia 100 lakini atakuwepo kwenye mechi ya Liverpool" Alisema kocha huyo.

Kabla ya Liverpool watawakaribisha Southampton ambao wako nafasi ya nane, ambao wiki iliyopita walipata ushindi wa  4-0 dhidi ya Newcastle.Kocha huyo raia wa Chile aliendelea kutoa taarifa pia za beki wa kulia,Muingereza Micar Richards kuwa amepona na amerejea kikosini.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!