Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Kocha mkuu wa Sochaux Herve Renard na kocha wa Al Ittihad ya
Alexandria Denis Lavange ni miongoni mwa walioorodheshwa kwa nafasi ya
kocha wa Al Ahly msimu ujao, taarifa zimeenea.
Ripoti nchini Misri zinasema kocha wa Al Ahly Mohamed Yousef ataondoka baada ya mwisho wa msimu huu.Tetesi zinasema Wafaransa hao wa wili ndio wanaoongoza kwenye orodha ya
Al Ahly na kwamba wataanza mashauriano mara moja kutaka kuwachukua.
Tetesi hizo pia zimedokeza kwamba Lavange anakaribia sana kuchukua kazi
hiyo baada ya kukataa kutia saini upya mkataba wake wa sasa ambao
unaisha baada ya miezi miwili.
Lavange alichukua usukani Al Ittihad na kuimarisha sana klabu hiyo,
na kwa sasa pia anasakwa na mabingwa wa Saudi Arabia Al Naser.
4 April 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment