ADEBAYOR AMEREJEA KIKOSINI.
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Emmanuel Adebayor na Vlad Chiriches wote wamerejea kwenye kikosi cha Tottenham Hotspurs na watakuwa tayari kuelekea mechi yao ya siku ya jumatatu dhidi ya timu ya Sunderland, hii itakuwa ni mechi ambao watoto hao kutoka jiji la London wataitumia kusahau kichapo cha mabao 4-0 walichopewa na Liverpool .
Mfungaji bora wa Spurs,Adebayor amekosa mechi mbili za ligi akisumbuliwa na misuli huku beki wa kati Chiriches,naye amekuwa nje ya kikosi tangu mwezi January akiwa na tatizo la kifundo cha mguu.
Kurudi wa beki huyo raia wa Romania itakuwa ni msaada mkubwa kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo kufuatia mapungufu yaliyojidhihirisha kwenye mchezo wao pale Anfield,kutokanana na matokeo mabaya ya timu hiyo,tayari ndoto zao za kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao kuanza kuyeyuka.
Tayari wako nyuma kwa anayeshika nafasi ya 5 timu ya Everton wakiwa pia na mechi moja mkononi na alama 8 nyuma ya timu yao ya Arsenal wanaoshika nafasi ya 4 kwenye msimamo wa ligi kuu.
"Hii ni wiki ngumu ," Sherwood amewaambia wanahabari .
"wote tumehuzunishwa na matokeo dhidi yaLiverpool. Tumejipanga vizuri na namna ya pekee ya kuonyesha hilo ni kushinda mechi yetu ya jumatatu." alisema kocha huyo.
Beki wa kati Jan Vertonghen na striker Roberto Soldado wote hawatokuwepo kuelekea mchezo huo pamoja na majeruhi wa muda mrefu Kyle Walker na Erik Lamela.
Sunderland wanahangaika kukwepa rungu la kushuka daraja na kwa sasa wapo nafasi ya 19, alama 4 pungufu dhidi ya anayeshika nafasi ya 17,timu ya West Bromwich Albion huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
0 comments:
Post a Comment