BENTEKE KULIKOSA KOMBE LA DUNIA
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Straika wa Ubelgiji Christian Benteke hatacheza Kombe la Dunia baada ya kubainika kwamba atakaa nje ya mchezo miezi sita kutokana na jeraha la kano za kisigino ambalo alipata akifanya mazoezi Alhamisi, klabu yake ya Aston Villa imesema.
"Ni pigo kubwa kwa Christian na kwa klabu,” meneja wa Villa Paul Lambert alisema kwenye tovuti ya klabu hiyo ya Ligi ya Premia (www.avfc.co.uk).
"Atakosa kipindi kilichosalia cha msimu, na bila shaka, Kombe la Dunia. Lakini atatia bidii sana kupata nafuu kwa sababu hiyo ndiyo kawaida yake na atarudi akiwa na nguvu zaidi kucheza msimu ujao.”
0 comments:
Post a Comment