Searching...
Image and video hosting by TinyPic
4 April 2014
Friday, April 04, 2014

HIKI NDICHO KINACHOENDELEA JUU YA ADHABU YA BARCELONA



 Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Barcelona watakata rufaa kupinga kufungiwa mwaka mmoja kutonunua wachezaji adgabu ambayo waliwekewa na Fifa kwa kukiuka “vikali” kanuni zilizowekwa kuhusu ununuzi wa wachezaji wachanga, klabu hiyo ilitangaza Jumatano. 

Adhabu hiyo inahusiana na ununuzi wa wachezaji 10 wasiotimiza umri wa miaka 18 kati ya 2009 na 2013 huku shirikisho hilo linalosimamia soka duniani, pia likipata Shirikisho la Soka la Uhispania (RFEF) na hatua ya kutofuata kanuni. 

"FC Barcelona watawasilisha rufaa kwa Fifa na haja ikiwepo, kesi itapelekwa kwa Mahakama ya Utatuzi wa Mizozo ya Michezo (CAS),” klabu hiyo ilisema kuptiia taarifa kwenye tovuti yake. 

“Klabu hiyo itaomba kuchukuliwe hatua za tahadhari ambazo zitadumisha haki za klabu, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa wachezaji vipindi vya kuhama achezaji.” 

Rufaa hiyo sharti iwasilishwe kwa Kamati ya Rufaa ya Fifa katika muda wa siku tatu na klabu hiyo inaweza kuwasilisha kesi hiyo kwa CAS kama hatua ya mwisho.
Adhabu hiyo ni pigo kuu kwa sura ya klabu hiyo iliyokubalika zaidi ulaya karne ya 21 baada ya madai ya kukwepa ulipaji ushuru wakati wa ununuzi wa nyota wa Brazil Neymar. 

Hata hivyo, kwenye taarifa ndefu iliyotolewa kwenye tovuti yao, klabu hiyo ilitetea njia yao ya ukufunzi na kufundisha wachezaji wasiotimiza miaka 18 ambao wanafika kwenye klabu hiyo.
Chini ya kanuni za Fifa mchezaji wa chini ya miaka 18 anaweza tu kuhamishwa ikiwa wazazi wake wamehamia taifa husika; kuhama huko hukubaliwa kwenye Muungano wa Ulaya ikiwa mchezaji ni wa kati ya miaka 18 kurudi nyuma; au nyumbani kwa mchezaji kuwe si zaidi ya kilomita 50 (maili 31) kutoka kwa mpaka wa kimataifa ambao atavuka. 

Barcelona walijitetea kwamba Fifa ilikosa kuangalia manufaa ya kimasomo ambayo wachezaji hao hujivunia katika academia inayosifika duniani ya La Masia.
"Mfumo huo wa La Masia huunganisha mafunzo ya uchezaji na elimu, malazi, chakula, usaidizi wa kimatibabu, mahitaji maalum ya watoto na mipango ya ukuaji kimichezo. 

"FC Barcelona hutengeneza watu kabla yao kuwa wachezaji, jambo ambalo halijazingatiwa na Fifa, ambayo ilitoa adhabu huku ikipuuza jukumu la kielimu la mpango wetu wa utoaji mafunzo.”
Ikidumishwa, adhabu hiyo inaweza kuathiri sana Barcelona kwani hawataweza kununua wachezaji wa kujaza nafasi za vigogo Victor Valdes na Carles Puyol ambao wamesema wataondoka klabu hiyo Juni.

Februari mwaka jana, Fifa iliwazuia wachezaji 10 husika; Lee Seung-Woo, Paik Seung-Ho na Jang Gyeol-Hee kutoka Korea Kusini, Patrice Sousia wa Cameroon, Mfaransa Theo Chendri na Bobby Adekanye, tineja Mnigeria na Mholanzi dhidi ya kushiriki mechi za ushindani.
Kando na adhabu hiyo ya kutonunua wachezaji, Fifa pia iliipiga Barcelona faini ya €369 000.
Mabingwa hao wa Uhispania walipatiwa siku 90 kurasmisha masuala kuhusu wachezaji hao 10 husika.

0 comments:

Post a Comment

:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Back to top!
Enjoy this page? Like us on Facebook!)