UKIFANYA KAMA KOCHA PULIS,WABONGO WATAKUMALIZA.
Na Oscar Oscar Jr
+255789784858
Meneja wa Crystal Palace kutoka Wales Tony Pulis anaitaka sana Cardiff City waponyoke kushushwa daraja kutoka Ligi ya Premia ingawa timu yake inakutana nao kwenye vita muhimu vya kukwepa kushuka daraja huko Wales Kusini Jumamosi wiki hii.
Klabu hizo mbili zilipandishwa daraja msimu uliopita kutoka Championship na huku Palace wakiwa alama tano juu ya eneo hatari, Cardiff wamepungukiwa na alama tatu kufika eneo salama wakiwa nambari 18.
Palace walijipatia nafasi murua ya kukwepa panga hilo baada ya kuwashangaza Chelsea kwa usindi wa 1-0 wikendi iliyopita lakini Cardiff wamekuwa na wakati mgumu kutafuta alama na kuendeleza matokeo mazuri tangu Ole Gunnar Solskjaer achukue nafasi ya Malky Mackay Januari.
"Lilikuwa jambo la kufurahisha sana kuona Cardiff wakipandishwa ngazi mwaka jana,” Pulis aliambia kikao cha wanahabari Alhamisi kabla ya mechi hiyo.
“Ulikuwa mwaka mzuri kwa soka ya Wales (Swansea pia walishinda League Cup) na ninataka inusurike. Ni klabu nzuri, kutoka jiji zuri na natumai kwamba watasalia Ligi ya Premia pamoja nasi.”
Pulis amefanya vyema Selhurst Park tangu atue huko Novemba kufuatia kuondoka kwa Ian Holloway.
Palace walikuwa wamekwama nambari 19 wakati huo lakini baada ya kushinda mechi saba na kutoka sare tatu kwenye mechi 19 wamepanda hadi nambari 16 kwenye jedwali na wana nafasi nzuri sana ya kujivunia msimu wa pili kwenye Ligi ya Premia kwa mara ya kwanza.
Palace walishushwa ngazi kutoka Ligi ya Premia msimu wa kuzinduliwa kwake 1992-93 na kila waliposhushwa ngazi tangu wakati huo - 1994-95, 1997-98 na 2004-05 – walishindwa kunusurika na kurudi walimotoka.
Baada ya timu yake kushindwa na Palace wiki jana, meneja wa Chelsea Jose Mourinho alisema Pulis anafaa kushinda tuzo ya Meneja wa Mwaka kama ataweka hai timu hiyo ya London, na mzaliwia huyo wa Wales alifanya mzaha na kusema: “Anajua analosema.”
Pulis pia aliwasifu wachezaji wake kwa kusikia ushauri wake.
"Kwa Mourinho kuchukua wakati wake na kupongeza vijana wetu, ni jambo kuu sana kutoka kwake kama mtu na meneja,” Pulis akaongeza.
"Pongezi kuu zaidi ambazo ninaweza kuwapa wachezaji wangu ni kwa moyo wao na umoja wao. Wamekuwa wazuri ajabu.
“Lakini lazima tuendelee kusonga mbele hadi tuhakikishe kwamba tuko salama kabisa.”
Aliongeza kuwa mashauriano na kipa Julian Speroni na wachezaji wengine ambao wanamaliza mikataba yao yangeanza “punde tutakapojua tutacheza ligi gani”.
0 comments:
Post a Comment