Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 March 2014
Sunday, March 30, 2014

MARCO REUS AIKARIBISHA REAL MADRID KWA HAT-TRICK



Mjerumani Marco Reus amesisitiza kuwa kujikwamua kwa Borussia Dortmund na kushinda 3-2 wakiwa VfB Stuttgart kuliipa timu hiyo ya Bundesliga imani zaidi kabla ya pambano la robofainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano ugenini Real Madrid. 

Stuttgart wanaokabiliwa na hatari ya kushuka daraja walipata uongozi wa 2-0 baada ya dakika 19 pekee wakati wa mechi hiyo ya Bundesliga Jumamosi, lakini Dortmund walijikwamua, huku Reus akifunga mabao matatu. 

Alama hizo tatu ziliwaweka Borussia kwenye nafasi ya pili nyuma ya mabingwa wapya wa Bundesliga Bayern Munich.
Dortmund ambao walishindwa kwenye fainali msimu uliopita, wanakabiliwa na mlima wa Real nkatika uwanja wa Bernabeu kabla ya mechi ya marudiano Aprili 8. 

Straika wa Poland Robert Lewandowski, mchezaji wa kwanza kufunga mabao manne nusufainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Dortmund waliporarua Real 4-1 msimu uliopita, haruhusiwi kucheza mechi hiyo ya Madrid, lakini Reus anasema timu yake lazima ijipe moyo kutokana na kujikwamua kwao mechi hiyo ya Jumamosi. 

"Bila kujali hata mechi hiyo ya Real, ilikuwa muhimu sana kujipa imani. Sasa tunajua kwamba tunaweza kujikwamua hata tukiwa magoli mawili chini,” Reus mwenye miaka 24 alisema.

“Tumethibitishia wakosoaji wetu kwamba tunaweza kushinda kabla ya mechi za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. 
 “Tulilala dakika chache za kwanza na 2-0 ilituamsha.” 

Dortmund wameshindwa mara nne mkesha wa mechi za Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Bundesliga na wameshindwa mechi tatu kati ya nane walizocheza Ligi ya Mabingwa kabla ya kufika fainali.
Reus huenda atachukua nafasi ya Lewandowski mbele wakiwa Madrid na Dortmund tayari watakosa beki wa kushoto wa Ujerumani Marcel Schmelzer, ambaye ana jeraha la mtoki, na kiungo wa kati mkabaji Sven Bender, ambaye ana jeraha la nyonga.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!