EVERTON WASHINDA NA KUWAKARIBIA ARSENAL
Kevin Mirallas na Steven Naismith walitoka benchi na kufunga na kuiwezesha Everton kushinda 3-1 dhidi ya Fulham inayoshika mkia kwenye ligi Jumapili na kupunguza mwanya kati yao ya timu nne bora za Ligi ya Premia hadi alama nne.
Everton walichukua uongozi wa dakika ya 50 Craven Cottage pale kipa wa Fulham David Stockdale alipoelekeza kombora la Naismith hadi kwenye lango lake bila kukusudia na akajifunga.
Ashkan Dejagah alitoa benchi na kufunga bao la kushangaza la kusawazishia Fulham dakika 71, kwa kuingia ndani kutoka winga ya kushoto na kutuma kombora ambalo liliingia golini kupitia kona ya juu upande wa kushoto.
Mirallas alirejesha uongozi wa Everton dakika nane baadaye, hata hivyo, kwa kufikia pasi ya nguvu mpya mwenzake Aiden McGeady na kwa utulivu akambwaga Stockdale, kabla ya Naismith kuumiza wageni hao kwa bao la tatu dakika ya 87.
Ushindi ulifanya timu hiyo ya Roberto Martinez kukaribia sana Arsenal walio nambari nne, wakiwa na mechi moja ambayo hawajacheza, kabla ya timu hizo mbili kukutana wikendi ijayo Goodison Park.
Uwezekano wa Fulham kukwepa kushushwa ngazi sasa ni kama hauko, kwani wamesalia alama tano kutoka eneo salama kukiwa na mechi sita pekee za kuchezwa.
0 comments:
Post a Comment