Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesisitiza nia yake ni kubakia
kama kiongozi wa klabu hiyo ya Uingereza kwa muda licha ya kutosaini
mkataba mpya na timu hiyo ya London.
Wenger aliongoza mechi yake ya 1000 Jumamosi dhidi ya Chelsea ingawa hatua hiyo iliishia kwa majonzi pale walipoadhibiwa 6-0.
Meneja huyo amepanga kumaliza sintofahamu ya hatima yake Arsenal kwa kuhakikishia ataendelea kushikilia usukani msimu ujao.
“Ndio, nafikiria hivyo,” alijibu alipoulizwa na wanahabari kama angekuwa mwalimu wa Arsenal msimu ujao.
“Nataka kupata ufanisi na matarajio ni mengi hapa ingawa kuna
wasiwasi inayotanda. Ahadi yangu ni kamili na sina nia ya kuangalia
kwingine. Nataka kubakia hapa na hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi.
“Hamu yangu ni kubaki hapa.”
Wenger aliteuliwa kama mwalimu wa klabu hiyo mwaka wa 1996 na
ameshinda mataji 11 na timu hiyo lakini hakafanikiwa kutia lolote
kibindoni tangu 2005 pale alipoongoza Arsenal kuinua kombe la FA.
WENGER HAENDI KOKOTE
Home
»
Unlabelled
» WENGER HAENDI KOKOTE
Share This To :
0 comments:
Post a Comment