Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 March 2014
Sunday, March 30, 2014

THIAGO ALCANTARA KUIKOSA MAN UNITED.



Kiungo wa kati wa Bayern Munich kutoka Uhispania Thiago Alcantara hatacheza mechi ya kwanza ya robofainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Jumanne dhidi ya Manchester United na anatarajiwa kutocheza wiki nne zijazo baada ya kupata jeraha la goti. 

Kocha wa Bayern Pep Guardiola aliwaambia Sky Sports kwamba mchezaji huyo wa miaka 22 huenda akahitaji kufanyiwa upasuaji baada ya kuraruka kiasi kano zake za goti la kushoto wakati wa mechi yao ya  Bundesliga nyumbani dhidi ya Hoffenheim Jumamosi. 

"Tutamkosa Thiago, ni mchezaji mzuri sana safu ya kati,” akasema Guardiola.
Jeraha hilo lina maana kuwa Thiago hatacheza mechi hiyo ya kwanza Jumanne Old Trafford na pia mechi ya marudiani uwanja wa Munich wa Allianz Arena Aprili 9. 

Nyota huyo wa Uhispania pia atakabiliwa na kibarua cha kupona upesi ndipo acheze nusufainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwishoni mwa Aprili, kama Bayern watasonga mbele. 
Mabingwa hao wa Ujerumani na Ulaya wanasubiri ripoti kamili baada ya uchunguzi Jumapili. 

Thiago, aliyejiunga na Bayern kutoka Barcelona Julai, alichechemea hadi nje ya uwanja baada ya dakika 25 uwanjani na nafasi yake ikachukuliwa na Philipp Lahm, mmoja wa nyota kadha waliokuwa wamepumzishwa kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya Manchester. 

Licha ya matokeo ya mechi hiyo, Bayern bado wako alama 22 mbele kwenye jedwali na waliongeza rekodi yao ya kutoshindwa Bundesliga hadi mechi 53.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!