Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 March 2014
Monday, March 31, 2014

SABABU 5 ZA MAFANIKIO YA LIVERPOOL MSIMU HUU.




Ushindi wa Liverpool wa bao  4-0 dhidi ya Tottenham Hotspur mwishoni mwa juma,umewapeleka Liverpool hadi nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza na kuibua hisia na matumaini kuwa,kuna uwezekano timu hiyo ikaweza kutwaa Ubingwa msimu huu ambapo kwa mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa mwaka 1990.

Mbio hizi za kuelekea ubingwa zimechangiwa na manager Brendan Rodger, ambaye alishuhudia timu hiyo ikimaliza nafasi ya 7 msimu wake wa kwanza tangu alipotwaa mikoba ya kuinoa timu hiyo ambayo ilikuwa na mtangulizi wake kocha Kenny Dalglish mwezi July 2012.
Kwa mujibu wa AFP Sports hizi ni baadhi ya mbinu zilizopelekea Anfield irejeshe matumaini ya kutwaa ubingwa na kurejesha furaha iliyopotea kwa muda mrefu chini ya kocha Brendan Rodgers mwenye umri wa miaka 41.

1. STAILI YA UCHEZAJI
 
Liverpool wamekuwa ni timu ya kucheza mpira wa pasi lakini,mfumo huo ulipotea tangu ujio wa Ken Dalglish ambaye alikuja kuinoa timu hiyo kwa mara ya pili,aina hiyo iliharibiwa na usajili wa rekodi kwenye timu hiyo wa euros 42.4 kwa Andy Carroll mwezi januari 2011. 

Rodgers amefanikiwa kuirejesha Liverpool kwenye mizizi yake,wanamiliki mpira ,amewaondoa hofu wachezaji wake na kuwafanya waweze kucheza pasi za nyuma na kwenda mbele hata kama wako wanakabiriwa na presha kiasi gani.  

"Kipindi cha makocha wengine,tulikuwa tunalazimika kuupeleka tu mpira mbele lakini mambo ni tofauti na zama hizi za Rodgers." Nahodha Steven Gerrard aliliambia gazeti la FourFourTwo mwaka jana. "Lakini  Brendan anatutaka tucheze kuanzia nyuma na kutumia zaidi pembe za uwanja kwa kasi na kumiliki mpira.Huu ndiyo mpango A anaotaka tucheze." 

2. USAJIRI WENYE TIJA
Misimu minne bila kushiriki klabu bingwa Ulaya,imepelekea klabu kuingia mfukoni na kusajili na katika hili,Rodgers amesaidia kwa kuona mbali kwenye dirisha la usajili.

Daniel Sturridge ameigharimu Liverpool £12 million tu kutoka Chelsea msimu uliopita katika dirisha dogo la mwezi januari na sasa ameibuka kuwa mmoja wa washambuliaji hodari wa England,amefunga magoli 34 kwenye mechi 43 alizoichezea Liverpool.

Kiungo mbrazilia Philippe Coutinho,alinunuliwa kutoka klabu ya Inter Milan kwa  £8.5 million, ameweza kuisaidia timu kufika hapo ilipo,japokuwa kati ya wachezaji 6 walionunuliwa msimu huu,ni golikipa tu Simon Mignolet ambaye amepata nafasi ya kudumu katika kikosi hicho. 

3. KUMTULIZA LUIZ SUAREZ
 
Kuna muda wakati msimu uliopita unamalizika,matumaini ya kumuona Luis Suarez ndani ya jezi ya Liverpool yalianza kufifia.Baada ya kufungiwa mechi 10 kwa kosa la kumng'ata beki wa chelsea,Branislav Ivanovic, mshambuliaji huyo wa Uruguay alivilalamikia vyombo vya habari vya Uingereza na kuwatuhumu Liverpool kwa kukataa ofa yake ya kujiunga na Arsenal wakati ilikuwa ni sehemu ya makubaliano yao.

Rodgers alisimama imara, na Suarez akaamua kumpa zawadi kocha huyo ya kufunga magoli 29 mpaka sasa msimu huu na kutengeneza muunganiko mzuri sana na Sturridge.Suarez alikubali kuongeza mkataba mpya mwezi disemba na anapigiwa upatu wa kuchaguliwa kama mchezaji bora wa mwaka wa EPL msimu huu.

4. MATUMIZI MAZURI YA KIKOSI.
Raheem Sterling kama si Rodgers huenda angepotea kabisa baada ya kuwa na msimu mbaya sana mwaka jana na ilifikia kipindi akawa mchezaji wa benchi tu lakini,mwanaume Brendan Rodgers ameweza kumtengeneza kijana huyo 19 na kuwa moja ya mawinga wazuri kwa sasa.Baada ya kuwa na mwanzo ambao si mzuri sana akiwa Anfield,mchezaji wa zamani wa Sunderland Jordan Handerson amekuwa bora kabisa chini ya uongozi wa Rodgers wakati,beki 21 Jon Flanagan ameibuka kuwa chipukizi hatari na kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

5. MBINU ZA UWANJANI NA MABADILIKO.

Rodgers alijifunza mbinu za mchezo wa soka kwa Jose Mourinho pale alipokuwa kocha wa timu ya vijana wakati Mourinho akiwa kama kocha mkuu wa Chelsea msimu wa 2005/2006 na 2006/2007,na kwa sasa anaonekana kuwa mtaalamu wa mambo mengi sana. 

Liverpool imetumia mbinu ambayo ni ngumu sana kwenye soka la kisasa msimu huu,mfumo wa 3-4-1-2 na baadae,wamekuwa wakibadili aidha 4-3-3 au 4-3-1-2 . 

Akionge baada ya mechi ya ushindi dhidi ya Spurs siku ya jumapili,Rodgers alisema: "Mechi zetu nne zilizopita,tulitumia mfumo wa  (4-3-1-2); na leo tumetumia 4-3-3.Tunafanya mabadiliko na hicho ndicho tunachokitaka na wachezaji hawana tatizo kuhusiana na jambo hilo. 

Kitendo cha kuwatumia washambuliaji wawili,kimewafanya kuweza kufunga magoli 88 kwenye msimu huu katika mechi 32 na katika hilo,Steven Gerrard 33 amekuwa muhimili sehemu ya kiungo mkabaji ambayo ni majukumu mapya msimu huu aliyopewa na Brendan Rodgers.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!