Historia itaandikikwa katika ligi ya Ujerumani ya Bundesliga ikiwa Hamburg watashushwa daraja kutoka shindano hilo baada ya kichapo cha 3-1 ugenini Borussia Moenchengladbach Jumapili mchezo huo uliwaacha nafasi ya pili kutoka mkiani.
Hamburg ni klabu pekee katika Bundesliga ambao hawajawahi shuka hadhi lakini wamesalia na mechi sita pekee kujiokoa baada ya kupoteza mechi 10 kati ya 15 za mwisho kwenye ligi hiyo.
Kiungo wa kulia kutoka Cameroon Jacques Zoua aliipatia Hamburg uongozi katika kipindi cha kwanza lakini Borussia walisawazisha kupitia penalti iliyopachikwa wavuni na nahodha wao Filip Daems baada ya kipa Rene Adler kuokoa mkwaju wake wa kwanza.
Mshambuliaji wa Brazil, Raffael na beki wa kati Alvaro Dominguez, waliongeza mawili dakika tano za mwisho kukamilisha ushindi huo ulifanya Hamburg kuchukua nafasi ya VfB Stuttgart waliopoteza 3-2 nyumbani dhidi ya Dortmund kwa wingi wa mabao.
Kocha Mirko Slomka ni mwalimu wa tatu msimu huu Hamburg baada ya Bert van Marwijk kupigwa chini Februari na mtangulizi wake Thorsten Fink akifutwa Septemba mwaka jana.
Kwingineko, Werder Bremen walishinda 2-1 dhidi ya Hannover 96 huku mabingwa Bayern wakitoka sare ya 3-3 dhidi ya Hoffenheim nyumbani na kuangusha alama kwa mara ya tatu pekee msimu huu.
0 comments:
Post a Comment