Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 March 2014
Monday, March 24, 2014

MOYES AMEJIANDAA KUISAMBARATISHA MAN CITY



Meneja wa Manchester United, David Moyes, amepigia upatu klabu yake kuwa ikitatamba Jumanne watakapo wakaribisha majirani zao na watana wa jadi Manchester City katika uwanja wao wa Old Trafford katika kivumbi cha ligi ya Premier. 

Moyes alinogeshwa na ushindi wao wa 2-0 ugenini West Ham United Jumamosi na ametangaza kuwa ni ishara kuwa vijana wake wanaimarika katika wakati unaofaa. 

City wanazuru Old Trafford wakiwa alama 12 mbele ya mabingwa hao waliodorora msimu huu na waliweza kuwaadhibu United 4-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza katika uwanja wa Etihad Septemba mwaka uliyopita. 

Waliendeleza harakati zao za kurithi maasimu wao kama mabingwa pale walipowacharaza Fulham 5-0 kabla ya United kujibwaga uwanjani na kuichakaza West Ham 2-0 huku kiungo Michael Carrick akicheza kama beki wa kati wa dharura kutokana na majeraha yaliyoikumba timu hiyo ya Moyes. 

Wawili hao watakosa washambuliaji wa kutegemewa, Robin Van Persie na Sergio Aguero, wanao uguza majeraha huku United wakitazamia kukosa walinda ngome muhimu, Rio Ferdinand, Johnny Evans na Chris Smalling. 

“Unaweza ona kuwa tunacheza bora zaidi na imani inarejea pole pole. Tutaendelea kudhihirisha mtindo huo.
“Tulifunga matatu dhidi ya West Bromwich na Olympiakos na tumepata magoli mengine mawili hapa na wachezaji ambao hawakuonyesha uwezo wao awali katika msimu huu wanaendelea kushamiri,” Moyes alisema.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!