Refa Andre Marriner huenda
akawekwa kando kwenye michezo ya mwishoni mwa juma baada ya kufanya
makosa kwenye michuano ya ligi kuu kumwondoa kimakosa mchezaji wa
Arsenal wakati timu hiyo ilipopoteza mchezo kwa kuchapwa magoli 6-0 na
Chelsea.
Oxlade-Chamberlain alionekana akimwambia Refa kuwa yeye ndiye aliyeshika mpira, hata hivyo uamuzi wa awali ndio ulikua wa mwisho.
Hata hivyo baadae Mariner alikiri na kuomba radhi kwa makosa yaliyojitokeza, akikiri kufanya makosa kutomtambua aliyepaswa kuadhibiwa katika mchezo huo.
Chama cha waamuzi wa mchezo wa kulipwa kimesema kuwa matukio ya kumwadhibu mchezaji kimamkosa ni nadra kutokea na mara nyingi husababishwa na sababu mbalimbali za kiufundi
0 comments:
Post a Comment