Difenda wa kati wa Bayern Munich Dante ameongeza mkataba wake katika
klabu hiyo iliyoshinda mataji matatu msimu uliopita, na sasa atakaa huko
hadi 2017, klabu hiyo ilisema Jumatatu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil, aliyejiunga nao kutoka Borussia
Moenchengladbach mwaka 2012, alijivunia ufanisi mkubwa msimu wake wa
kwanza kwa kushinda Bundesliga na German Cup na pia Ligi ya Klabu Bingwa
Ulaya.
"Dante amekuwa bila shaka mmoja wa wachezaji wazuri zaidi tulionunua
miaka ya hivi majuzi,” alisema afisa mkuu mtendaji Karl-Heinz Rummenigge
kupitia taarifa. "Amekua na kuwa mmoja wa wachezaji wetu muhimu zaidi
uwanjani nan je ya uwanja.”
Mchezaji huyo wa miaka 30 aliitwa mara ya kwanza kuchezea Brazil
mwaka jana na anatumai kwamba atapata fursa ya kucheza Kombe la Dunia
litakalochezewa kwao Juni.
Bayern, ambao watakutana na Manchester United katika robofainali Ligi
ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi ujao, watatwaa taji la Bundesliga leo Jumanne
kama watashinda Hertha Berlin.
25 March 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment