Shirikisho la kandanda barani Uropa, Uefa, limewatoza miamba wa
Ujerumani Bayern Munich, faini ya Euro 10,000 (Dola 13,774 za Marekani)
na kuwaamuru wafunge sehemu ya uwanja wao kwenye robo fainali ya
Champions League dhidi ya Manchester United kutokana na kupeperushwa kwa
bango lenye maandishi machafu.
Adhabu hiyo ilitolewa baada ya mashabiki wa mabingwa wa kombe hilo
kuonyesha bango lililo andikwa ‘Gay Gunners’ kwa kimombo lililo kejeli
Arsenal kuwa ni timu ya mashoga kwenye mechi ya marudiano katika awamu ya
16-bora ya shindano hilo lililokamilika kwa sare ya 1-1.
Bayern imepangwa kucheza na timu ya David Moyes,Manchester United kwenye robo fainali huku mkondo wa kwanza
ukisakatwa Aprili mosi na marudiano yakichezwa Munich Aprili 9.
Kwenye taarifa, kamati ya mwelekeo na nidhamu ya Uefa, imeamuru kufungwa kwa sehemu ya uwanja wa Allianz Arena jijini Munich.
Klabu hiyo ilionywa kuwa marudio ya tukio kama hilo itawagharimu faini ya Euro 50,000 na mechi kuchezwa bila mashabiki wowote.
“Tunajuta tukio hilo katika mechi yetu na Arsenal na tunajitenga na
bango hilo la hujuma. FC Bayern haitokubali kamwe kitendo kama hicho,”
mwenyekiti wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge, alisema
“Ni kwa majuto tunakubali adhabu ya Uefa.”
24 March 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment