Searching...
Image and video hosting by TinyPic
26 July 2013
Friday, July 26, 2013

NIONAVYO MIMI DAVID MOYES BADO ANASUMBULIWA NA MZIMU WA FERGIE

                                 
Tungekuwa huku kwetu,watu wangesema Sir Alex alimpendekeza David Moyes kwa sababu wote kwao kumoja.Unaposema kwamba David Moyes ni bonge la kocha,lazima uwe na vigezo na sio unazi tu.

Ninachokiamini Moyes atatolewa na man united lakini sio yeye kuitoa man united.Man u inajina kubwa kuliko yeye, wakati wataalamu wakisema united imepoteza BRAND yake baada ya SAF kuiacha,yeye ndo kazidi kula PROMO.

Hakuna chaajabu alichokifanya akiwa na Everton,sema tu watu tunajaribu kuamini kuwa pengine,walimu wakipata mshahara mkubwa,vifaa vya kufundishia,wakilipwa madeni yao na marupu rupu watoto wetu watapata elimu bora.Hii ni imani tu ambayo inaweza ikawa au isiwe.

Watu wataendelea kumkumbuka Sir Alex mpaka united itakapo kaa sawa.watu kama Del Bosque,Mourinho,Gaudiola,pellegrini,Ancelloti angalau ndo wanaendana na united.

Kama hatosajili vizuri,united itamshinda Moyes.Nadhani anahitaji kutulia sana na kuleta watu sahihi PELLEGRINI na MOURINHO watamsambaratisha.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!