Searching...
Image and video hosting by TinyPic
5 July 2013
Friday, July 05, 2013

YANGA WATUA MWANZA SALAMA.

                                                    



KIKOSI cha Mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC kimewasilimjini Mwanza mchana huu tayari kabisa kwa ziara yake ya wiki moja Kanda ya Ziwa inayoanza kesho kwa mchezo wake wa kirafiki dhidi ya mabingwa wa Uganda, KCC Uwanja wa CCM Kirumba.
 
Yanga iliyoondoka mchana wa leo ndege, inatarajiwa kufanya mazoezi mepesi Uwanja wa CCM Kirumba jioni ya leo tayari kabisa kujiandaa na mpambano huo wa hapo kesho.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts amesema anafurahi kupata nafasi hiyo ya kutembelea Kanda ya Ziwa, wapenzi na washabiki watapata fursa ya kuwaona wachezaji wao na kusherekea ubingwa.

Katika ziara hiyo, Yanga itacheza mechi tatu za kirafiki na baada ya kesho, itarudiana na KCC Jumapili Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga kabla ya Alhamisi kukamilisha ziara yake kwa kucheza na wenyeji Rhino FC, iliyopanda Ligi Kuu msimu huu Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi.

Yanga imetua Mwanza na msafara wa watu 34, wakiwemo wachezaji 23 na benchi la ufundi na viongozi watatu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!