Searching...
Image and video hosting by TinyPic
13 July 2013
Saturday, July 13, 2013

NIONAVYO MIMI WACHEZAJI WA KIBONGO HAWAJUI HESABU.



Inasemekana David Villa anahama FC Barcelona na kujiunga na Atletico Madrid.Sababu kubwa ya Villa ni kupata timu ambayo itampa nafasi ya kucheza mara kwa mara ili 2014 aweze kuitwa kwenye timu ya Taifa Kombe la Dunia huko Brazil.

Ukimsikiliza Thiago Alcantara atakwambia anataka kuhama FC Barcelona ili apate timu ya kucheza mara kwa mara na aweze kuwa sehemu ya kikosi cha Hispania 2014 kombe la Dunia.

Kina Uhuru suleyman,Said Bahanuzi,Nurdin Bakari n.k malengo yao huwa ni kucheza simba na yanga tu.Baada ya kutua moja ya hizi klabu,Wapo tayari wasicheze mechi hata moja katika maisha yao ili mradi tu wapo Simba au Yanga.

Hizi hesabu wangezipiga mwaka jana ili kujitafutia nafasi ya kucheza CHAN na kufuzu kwa kombe la Dunia.wenzetu hawajui hizi hesabu wamelala tu.

Watu wangu wa Mbeya mpo?? Leo napatikana MBEYA nimefika tangu asubuhi.nitakuwepo kwa siku mbili tu.Baridi balaaaa!!

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!