NIONAVYO MIMI KWENYE WIMBO WA TAIFA.
siku ya fainal ya Brazil vs Spain nilishuhudia shangwe,Tabasamu na mzuku wa hali ya juu toka kwa mashabiki wa Brazil wakati wakiimba wimbo wao wa TAIFA.
Ukiangalia walivyokuwa wanaimba,utagundua kwamba walikuwa wanamaanisha kile walichokifanya baada ya dk 90.
Nimekuwa nikienda uwanja wa TAIFA DAR ES SALAAM lakini ukweli ni kwamba,Watanzania wengi hawajui kuimba wimbo wa Taifa.
Hawajui beti ipi inatangulia kati ya "Mungu ibariki Tanzania" na,"Mungu ibariki Afrika" hivi jamani na hili linahitaji KATIBA MPYA?
Watanzania wamekuwa wakijitafuna midomo kila siku kwenye kuimba wimbo wa Taifa,kuna mambo ya kulaumu TFF,Media n.k ila kwa hili,ni wewe na mimi ndo wakulaumiwa.
0 comments:
Post a Comment