Searching...
Image and video hosting by TinyPic
18 July 2013
Thursday, July 18, 2013

NIONAVYO MIMI KWA MASHABIKI WA ARSENAL



Hawa watu bwana wanastahili pongezi,wanamsifia sana Jack Wilshere na kiukweli dogo anajua lakini,nadhani watu wanamsifia muda mwingi kuliko kumuona uwanjani.

Anakaa sana nje kwa majeruhi sasa sijui mnampimaje mchezaji ambae anacheza mechi 8 tu za ligi msimu mzima! Kuna uwezekano mkubwa kwamba kama JACK angekuwa muhispania,angekuwa hajawahi kuitwa timu ya Taifa.

Baada ya kushinda mechi ya maandalizi dhidi ya Indonesia 7-0 hahahaaa...mitandao ilichafuka kwa majigambo.Waliwaponda Man u,man c ambao wote walifungwa mechi zao za maandalizi.

Arsene wenger anajiandaa kusaini mkataba mpya na arsenal na kukamilisha kila kitu,mashabiki wanafurahi lakini wakishatandika 8-2 tena,matusi kibao yataelekezwa kwa mzee wenger.

Kwa idadi ya magoli,waliyopata arsenal mechi ya kwanza ilitakiwa kuwe na hat-trick 2 na goli moja hapo ndo angalau ningeona safu ya ushambuliaji imeimarika lakini,kila mtu na goli lake,bado sana.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!