KOCHA Manuel Pellegrini amemuorodhesha
Devante Cole katika kikosi chake cha Manchester City kwa ajili ya ziara
ya kujiandaa na msimu mpya Afrika Kusini.
Kinda huyo nyota wa City ni mtoto wa
mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa England na mahasimu wao, Man
United, Andy Cole na amekuwa akichezea timu ya akademi ya Etihad.
Kama baba, kama mwana: Devante Cole akiichezea Manchester City
Cole mdogo mwenye umri wa miaka 18,
amefuata karibu kila kitu kwa baba yake kichezaji – wepesi na kasi,
uchezaji, namna anavyopambana uwanjani na jinsi anavyolijua goli.
Pellegrini atakipeleka kikosi chake
kipya huko katika ziara ya mechi mbili Afrika Kusini kuanzia Julai 14
dhidi ya Supersport mjini Pretoria na kisha AmaZulu mjini Durban siku
nne baadaye.
Cole Mabao: Devante anafuata nyayo za baba yake, Andy ambaye alichezea Manchester City pia
0 comments:
Post a Comment