Mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ivory
Coast, aliyetimiza miaka 27 jana, anatuhimiwa kutumia leseni feki ya
udereva ya Ubelgiji na kufanya jithada za kupata leseni ya Uingereza.
Tiote, aliyesajiliwa The Magpies kutoka
FC Twente ya Uholanzi mwaka 2010, alisimamishwa na Polisi wa Northumbria
karibu na Uwanja wa mazoezi wa klabu yake Februari 12 kwa kushukiwa
kudanganya juu ya udereva wake.
Kanjanja: Tiote, akiwasili mahakamani
Mashitaka: Mchezaji wa Newcastle anakabiliwa na mashitaka matano
Gari la kiungo huyo, aina ya Chevrolet Camaro, lenye thamani ya Pauni 75,000, lilifikishwa kituo cha Polisi alipokamatwa.
Tiote sasa atatakiwa kufika rufaa katika Mahakama Kuu ya Newcastle Julai 5.
0 comments:
Post a Comment