Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 June 2013
Sunday, June 16, 2013

NIONAVYO MIMI STARS VS IVORY COAST


                                                                           


Kila Stars walipopata goli,nilijikuta nimevua shati huku nikibaki na vesti,asanteni sana Taifa Stars.Kama tungeshinda leo,nadhani ningevua kingine mbali na shati.

Tumefungwa 4-2 na Ivory Coast ambao nadhani wamepata walichokihitaji.Erasto nyoni leo kila akibandua Kalou,anakuja Gervinho.kapata tabu sana,Gervinho na Kalou wanambio na chenga hivyo,usidhani ni rahisi kuwakaba.


Magoli ya Ivory coast yamefungwa na Yaya Toure ambaye alifunga kwa mpira wa adhabu na la pili kwa mkwaju wa penalty,mengine yalifungwa na Traore na Wilfred Bonny alihitihisha kwa upande wa Tembo hao wa Afrika.Magoli ya TAIFA STARS yalifungwa na Amri kiemba na Thomas Ulimwengu.

Kila tulipopata goli tulikimbia na kushangilia wakati wao,kila walipofunga waliitana na kupeana maelekezo.

Nadhani kama tungekuwa na mpiga faulo wa uhakika,tungeweza pata matokeo mazuri.Kiungo hasa kipindi cha pili,ilikuwa poa sana.

Anyway,tumefanya kile ambacho tunakiweza.Timu yetu inazidi kuimarika siku hadi siku.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!