Aliyekuwa
golikipa wa timu ya Simba, Azam na Mtibwa Deogratius Munishi maarufu
kama Dida amejiunga rasmi na klabu bingwa ya Tanzania bara - Dar Young
African.
Kwa
mujibu wa mmoja wa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Abdallah Bin
Kleb ni kwamba Dida amesaini mkataba wa kuitumikia Yanga kwa miaka
miwili akiwa 'free agent' (mchezaji huru).
Dida
ambaye alisajiliwa na Azam akitokea Mtibwa na kuweza kujijengea nafasi
katika kikosi cha kwanza cha AZAM kabla ya miezi kadhaa iliyopita
kusimamishwa na wachezaji wenzie Erasto Nyoni, Said Morad, Aggrey Morris
kwa tuhuma za kupokea mlungura na kusababisha timu yao kufungwa na
Simba katika mchezo wa raundi ya kwanza wa ligi kuu msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment