Searching...
Image and video hosting by TinyPic
25 June 2013
Tuesday, June 25, 2013

NIONAVYO MIMI KASSEJA NENDA ZAKO RHINHO RANGERS



.Kuna taarifa kwamba KASSEJA hatakiwi tena mitaa ya msimbazi huku,NURDINI BAKARI nae yakimkuta hayo hayo mitaa ya Twiga na Jangwani.Rhino Rangers ya Tabora imepanda daraja na itarudi kutumia ALI HASSAN MWINYI STADIUM baada ya kuachwa na MILAMBO fc iliyoshuka daraja hapo siku za nyuma.

kwa namna jina la KASSEJA lilivyokuwa ni kama kampuni na niamini mimi,kuna watu wengi tu ambao siku wakishikana mikono na kasseja,wana weza wasinawe ili waendelee kubaki na harufu yake mkononi.HE IS THE SUPER STAR

RINHO andaeni pesa za kumsajili KASSEJA mtafaidika sana kupitia jina lake.Mkimpata andaeni tisheti,kofia,kalenda,nguo za ndani n.k. muwekeni kasseja kwenye gari lenye vifaa hivyo halafu nendeni nae Usoke,Mabama,Ulyankulu,Sikonge,Igunga,Nzega,Uyui na Urambo mtapiga pesa chafu sana pande hizo.

Tengenezeni duka la vifaa vyenu na muwatangazie mashabiki wenu kwamba kila jumapili asubuhi KASSEJA na NURDINI watakuwepo dukani hapo wakisaidia kutoa huduma,trust me,siku hiyo duka litafurika mpaka nje.Bidhaa zenu zianzie elfu 1,000 hadi 20,000 tosha.

kila siku mazoezini,wapeni fulsa mashabiki wenu kupiga picha na KASSEJA na NURDINI kwa kuichangia club yao shilingi elfu moja tu.watu wangu wa kanyenye,Kiloleni,Isevya,Uhindini,cheyo.Jamani hela za kumnunulia hazija rudi tu???

Simba wanamuona anagharama kubwa ni kwa sababu hawazalishi kupitia jina lake,ni kweli kuna uwezekana kiwango kimepungua kidogo ila kibiashara bado analipa sana.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!