Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 February 2015
Monday, February 02, 2015

Kane ajikita Spurs mpaka 2020




Na Chikoti Cico


Mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Hotspur Harry Kane amejikita kwenye klabu hiyo yenye maskani yake jijini la London baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na nusu na atapokea mshahara wa pauni 45,000. Mkataba huo mpya utamuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2020.

Kane mwenye umri wa miaka 20 amekuwa kwenye kiwango bora katika msimu huu huku akifunga jumla ya magoli 20 kwenye michezo 33 aliyoichezea klabu ya Spurs katika michuano mbalimbali, ambapo katika michezo 19 ya ligi kuu nchini Uingereza amefunga jumla ya magoli 10.

Baada ya kusaini mkataba huo mpya Kane aliuambia mtandao wa Spurs kwamba “imekuwa ni miezi sita mizuri, nimependezwa na jinsi mambo yalivyoenda. Huu (mkataba) ni hatua nyingine na natumai kwasasa nitafanya kazi tena kutokea hapo na kuendelea vizuri zaidi”.

Aliendelea kusema “ambacho unaweza kufanya kama mchezaji ni kujaribu kuwa bora na ndicho ninachikifanya kuwa bora, kufunga magoli zaidi na kucheza vizuri kwa ajili ya timu. Ninaangali mbele zaidi mpaka mwisho wa msimu”.

“Nina miaka 21 tu na nina michezo mingi mbele yangu, nitaendelea kucheza na kufanya kazi zaidi kwa ajili ya timu na kwa ajili ya klabu, nimekuwa hapa Spurs tangu nikiwa na miaka 11 na mara zote nimeipenda klabu, nimekuwa kwa miaka 10 hapa sasa na natumaini kuna miaka mingine mizuri inayokuja”



0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!