NYOTA wa Brazil, Neymar anaamini
Hispania inapewa nafasi kubwa ya kutwaa Kombe la Mabara katika Fainali
itakayopigwa leo, lakini amesema timu yake haiwahofii mabingwa hao wa
Ulaya na Dunia.
Hispania inaingia kwenye fainali hiyo leo, ikitazamiwa kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza na kuendeleza
mafanikio yao ya miaka ya karibuni katika soka, wakitwaa mfululizo
mataji ya Euro na Kombe la Dunia.
Mafanikio hayo yameifanya La Roja ishike
nafasi ya kwanza katika viwango vya soka duniani na licha ya kwamba
Brazil inapewa nafasi kutokana na kucheza nyumbani, Neymar amesema
kikosi cha Vicente Del Bosque ni tishio.
Mazoezi yanajenga usahihi: Neymar (katikati), ambaye hivi karibuni amesaini Barcelona, akiwa na mpira mguuni mwake
Pamoja na hayo, mshambuliaji huyo ambaye
atacheza Ligi Kuu ya Hispania msimu ujao baada ya kujiunga na Barcelona
mapema majira haya ya joto, pia ana matumaini na timu yake inaweza
kuweka rekodi ya kutwaa kwa mara ya tatu mfululizo Kombe la Mabara na
mara ya nne kwa ujumla.
"Wao (Hispania) ni timu nzuri duniani na wanapewa na nafasi,"alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.
"Lazima tucheze soka bila woga.
Tunacheza na timu bora duniani kwa sasa, lakini pia tuna wachezaji
wazuri katika timu ya taifa ya Brazil,".
Maelekezo: Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari (kulia) akizungumza na mshambuliaji wa zamani wa Everton na Man City, Jo
Kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari amesema kikosi chake kina uwezo wa kuibwaga Hispania.
"Tunacheza na Hispania tukiheshimu ubora wao, lakini pia kujaribu kuonyesha uwezo wetu na vipaji,"alisema.
"Tumefika Fainali na tuna ubora wa kutosha kuwabwaga,".
Nchi hizo mbili zinakutana kwa mara ya
kwanza tangu zitoke 0-0 katika mchezo wa kirafiki mjini Vigo mwaka 1999.
Mara ya mwisho, Hispania ilipokutana na Brazil Uwanja wa Maracana
walifungwa mabao 6-1 - mwaka 1950.
Samba: (kutoka kushoto) Marcelo, Oscar, Fred, Neymar, David Luiz na Hulk katika mazoezi ya Brazil mjini Rio
Timu zote zimeonyesha ni timu mwaka huu
katika Kombe la Mabara, Brazil ikishinda mechi zake zote nne hadi sasa,
wakati Hispania walishinda mechi zao zote tatu za kundi lao, kabla ya
kuing'oa kwa matuta Italia kwenye Nusu Fainali kali katikati ya wiki.
Andres Iniesta ataiongoza Hispania leo
Wamemaliza siku yao: Nyota wa Real Madrid, Marcelo (kulia) akiburuza kipozeo baada ya mazoezi huku Neymar akimuangalia
0 comments:
Post a Comment