PELLEGRINI SASA ATAKA KUMSAJILI FRED WA BRAZIL NA CARDOZO WA BENFICA KUTENGENEZA PACHA JIPYA HATARI LA USHAMBULIAJI MAN CITY
KOCHA wa Manchester City, Manuel
Pellegrini amehamishia mawindo yake kwa washambuliaji Mbrazil, Fred na
Oscar Cardozo wa Benfica, baada ya kuamua kuachana na Edinson Cavani aliyekuwa anatakiwa na kocha aliyemtangulia, Roberto Mancini aliyetimuliwa.
Pellegrini, ambaye amepewa kauli ya
mwisho kuhusu usajili katika klabu hiyo licha ya kuwepo kwa Mkurugenzi
wa Soka, Txiki Begiristain, hataki City ibomoe benki kwa ajili ya
Cavani, baada ya klabu yake, Napoli kukataa ofa iliyotolewa ya Pauni
Milioni 54.
Mchezaji Mkuu: Fred wa Brazil (kushoto) anatakiwa Manchester City
Anayewatoa udenda City: Oscar Cardozo anaweza kuchukua nafasi ya Carlos Tevez
Mshambuliaji wa Fluminense, Fred, ambaye
ataiongoza nchi yake leo katika Fainali ya Kombe la Mabara dhidi ya
Hispania, kwa sasa anatabirwa kwenda kuziba pengo la Carlos Tevez,
aliyejiunga na Juventus wiki iliyopita.
Fred, mwenye umri wa miaka 29, alifunga
wakati Brazil inatoa sare ya 2-2 na England mapema mwezi huu na akafunga
mabao mawili dhidi ya Italia katika michuano hii ya kupashia misuli
moto Kombe la Dunia inayofikia tamati leo.
Cardozo, mshambuliaji wa Montenegro,
Stevan Jovetic na Stephan El Shaarawy, wa AC Milan, pia wametajwa kama
wawania kurithi mikoba ya Tevez huku Pellegrini akitarajia kutengeneza
alama yake katika klabu hiyo kabla hajaanza mazoezi ya kujiandaaa na
msimu mpya.
Kwa muda mrefu, Mancini alimfanya
mshambuliaji wa Uruguay, Cavani chaguo la kwanza katika wachezaji
anaowataka, lakini akafukuzwa City siku kadhaa baada ya kufungwa kwenye
Fainali ya Kombe la FA na Wigan mwezi uliopita.
Pellegrini, ambaye aliiongoza Malaga
kutinga Robo Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, anataka
kuongeza mshambuliaji na na sentahafu, baada ya kukamilika kwa usajili
wa winga wa Hispania, Jesus Navas na kiungo wa Brazil, Fernandinho.
City inataka kukata Pauni Milioni 20
kumnunua beki wa kati wa Real Madrid, Pepe, ambaye atatengeneza
ushirikiano mpya na Vincent Kompany.
Mpango wao wa sasa kutaka kumsajili Pepe
ni pigo kubwa kwa beki wa sasa wa City, Joleon Lescott, ambaye
anatarajia kuwa na mazungumzo na klabu hivi karibuni juu ya mustakabali
wake.
Lescott, mwenye umri wa miaka 31,
anataka uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza, ili kulinda nafasi
yake katika kikosi cha timu ya taifa ya England, kuelekea Fainali za
Kombe la Dunia mwakani, Brazil.
0 comments:
Post a Comment