Klabu ya Albacente inayoshiriki kwenye ligi ya daraja la 2 nchini Spain maarufu Segunda Division B - ingeweza kushushwa daraja kama isingekuwa kusaidiwa na mchezaji wao wa zamani Andres Iniesta masaa 11 kabla ya muda muda waliopangiwa kulipa madeni ya mishahara ya wachezaji inayofikia kiasi cha €240,000.
Klabu hiyo ingeshushwa mpaka daraja la 3 kama wangeshindwa kulipa deni lao mpaka kufikia Ijumaa saa sita kamili mchana.
Japokuwa, Iniesta, ambaye ana hisa nyingi kuliko watu wote kwenye klabu hiyo ambayo pia ndio alianzia soka lake, alikuja kuokoa jahazi, kwa kulipa madeni yote ya mishahara kutoka kwenye mfuko wako.
Hii sio mara ya kwanza kwa kiungo huyo wa Barcelona kuisadia timu hiyo - mpaka sasa ameshalipa kiasi kipatacho cha €420,000 tangu 2011.
Iniesta, ambaye kwa sasa yupo Brazil, alicheza kwa miaka miwili katika klabu ya Albacente kabla ya kujiunga na Barcelona kwenye academy yao ya La Masia mwaka 1996.
0 comments:
Post a Comment