Searching...
Image and video hosting by TinyPic
24 June 2013
Monday, June 24, 2013

AZAM FC WATANGAZA KUANZA MAZOEZI.



Baada ya mapumziko ya wiki tano kikosi cha Azam FC kimeanza mazoezi rasmi leo kujiandaa naligi kuu ya vodacom 2013, katika mazoezi ya leo Azam FC iliwakosa wachezaji 16 kutokana na sababu mbalimbani.

waliokosekana ni wachezaji nane wa timu ya taifa Taifa Stars, wachezaji wanne wa kigeni ambao wameomba ruhusa ya kujiunga na wenzao wiki ijayo, David Mwantika aliye na matatizo ya kifamilia kama ilivyo kwa Omary Mtaki anayeuguza baba yake na Himid Mao aliyefiwa na baba yake mkubwa.

Waliohudhuria mazoezi ya kwanza leo ni Malika Ndeule, Brian Umony, Jabir Aziz stima, Waziri Salum, Gaudence Mwaikimba, Luckson Jonathan kakolaki, Samih Haji Nuhu, Seif Abdallah Karihe, Wandwi Jackson na Ibrahim Mwaipopo
Mchezaji pekee ambaye hakufika mazoezini na hakuna taarifa zozote juu ya kukosekana kwake ni Said Morad Mweda


Kwa mapenzi wa Azam FC na wanachama wa Azam FC Facebook page, mapumziko yamekwisha na timu sasa imerudi na kuanza maandalizi ya ligi, kaa tayari kwa taarifa kemkem kuhusu timu yetu kaa hapa hapa soka stadium.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!