YANGA KUTEMA NYOTA SABA
KLABU ya Yanga inatarajia kuwatema nyota wake sita katika msimu ujao wa ligi kuu na michuano ya kimataifa.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa, nyota hao wanatemwa kutokana na kushuka kwa viwango vyao.
Kwa mujibu wa habari hizo, miongoni mwa nyota hao sita, wamo watakaouzwa kwa mkopo kwa klabu zingine za ligi kuu.
Wachezaji hao ni pamoja na kipa Saidi Mohamed, mabeki Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Salum Telela, Ladslaus Mbogo, Stephano Mwasika na kiungo Nurdin Bakari.
Habari hizo zimeeleza kuwa, Mbogo anaachwa kutokana na kuwa mgonjwa kwa muda mrefu na hivyo kushindwa kuitumikia vyema timu hiyo katika ligi ya msimu uliopita.
Tangu alipojiunga na Yanga mwaka juzi, Mbogo ameshafanyiwa operesheni mara tatu kwa ajili ya kuondoa uvimbe kwenye shingo yake.
Wachezaji wanaotarajiwa kuuzwa kwa mkopo ni Nurdin na Saidi kwa vile bado wana mikataba ya kuitumikia Yanga.
Wakati huo huo, klabu ya Yanga imesema inatarajia kuwatangaza nyota wake wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao kabla ya timu hiyo kwenda Sudan.
Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga, Abdalla Bin Kleb alisema mjini Dar es Salaam juzi kuwa, wachezaji hao ni wale waliopendekezwa na Kocha Ernie Brandts kutoka Uholanzi.
"Tayari tunayo majina ya wachezaji wapya tuliowasajili kutokana na mapendekezo ya kocha na tunatarajia kuyatangaza wakati wowote wiki ijayo,"alisema.
Bin Kleb alisema kwa sasa wapo katika hatua za mwisho za mazungumzo na baadhi ya wachezaji hao wapya kabla ya kuingia nao mikataba.
Miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na Yanga ni pamoja na mshambuliaji Mrisho Ngasa, aliyekuwa akiichezea Simba kwa mkopo akitokea A zam.
30 May 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment