NA
JOACHIM SOLOGO
Habari wadau wa Blog yetu pendwa ya Soka Stadium. Leo nimeona ni vyema
tushirishane mada hii inayohusu udhamini wa vilabu vyetu hapa nchini. Ni muda
mrefu sasa nimekuwa nikifuatilia udhamini wa vilabu vyetu lakini ninaona kama
maigizo. Vilabu vingi vinavyoshiriki ligi kuu hapa nchini havina udhamini huku
vile vyenye udhamini ukionekana kutokidhi haja lakin pia ni wa magumashi. Hivi
ni nani anayepaswa kulaumiwa ktk jambo hili? Je ni vilabu au makampuni? Au je
ni TFF? Bado napata kigugumizi. Hivi ni kweli makampuni ya hapa nchini hayaoni
umuhimu wa kujitangaza kupitia vilabu vyetu? Au klabu zetu ni tajiri kiasi
kwamba hazihitaji udhamini wa makampuni haya?
Nilifika mbali zaidi na kujiuliza kama kuna
umuhimu wa klabu kuwa na mdhamini au kampuni kujitangaza kupitia club. Hivi ni
nani anayefaidika zaidi katika udhamini na kujitangaza, ni kampuni au club?
Toka mwaka jana nimeifuatilia kwa ukaribu club ya Simba katika suala la jezi
inazovaa, katika jezi za Simba nimeona kuna nembo ya Adidas. Swali la
kujiuliza, hivi kweli Simba wanadhaminiwa na adidas? Au wanavaa tu bila
kutambua kwamba wanaitangaza Adidas ambayo ni kampuni kubwa sana ya vifaa vya
michezo yenye maskani yake huko Marekani.
Ni wakati wa Watanzania kufumbua macho na
kuangalia namna ya kupata wadhamini kwa mikataba inayoeleweka, vilabu vingi
Duniani vimekuwa vikinufaika na udhamini wa makampuni tofauti duniani. Ndiyo
maana hivi karibuni umeshuhudia Man City wakibadili udhamini kutoka UMBRO
kwenda NIKE huku Arsenal nayo ikikamilisha udhamini kutoka NIKE kwenda PUMA.
Hayo yote yanatokana na vilabu kuangalia mdhamini anayetoa dau kubwa. Real
Madrid nao wameridhia kubadili mdhamini kutoka kampuni ya kamali ya Bwin kwenda
Fly Emirates ambayo ni kampuni kubwa ya usafiri wa ndege duniani kote.
Kwa mtazamo wangu ninaona tatizo kubwa la
klabu zetu kukosa udhamini ni uongozi mbovu. Kumekuwa na uongozi mbovu kutoka
Shirikisho la Soka hapa nchini (TFF) hadi ktk vilabu. Mnakumbuka sakata la
African Lyon kuhusu udhamini wao wa Zantel, TFF walifanya udhamin wa African
Lyon kuwa batili kwa sababu ya wao TFF kukurupuka ktk udhamini wao na Vodacom
na kujikuta wakiweka kipengele kinachozuia klabu kudhaminiwa na kampuni yenye
ushindani na Vodacom.
0 comments:
Post a Comment