Hatimaye BAYERN MUNICH wameweza kuwa mabingwa wapya tangu mwaka 2001 walipopata ubingwa huo.walifika Fainal kwa kumfunga bingwa mpya wa ITALY SERIA A,Juventus nyumbani na ugenini kwenye robo fainal na baadae,kumfunga FC BARCELONA timu bora kabisa barani ulaya nyumbani na ugenini.Hiki hakikuwa kitu kidogo.
Kijana wa kiholanzi aliyezaliwa mwaka 1984 ARJEN ROBEN baada ya kubadilishwa jina na kuitwa 'MZEE WA NUKSI KWENYE FAINAL' jana aliweza kufuta hilo jina baada ya kufanya kazi nzuri ya kuifungia timu yake goli la ushindi na kutoa pasi ya mwisho ya goli la kwanza alilofunga kijana wa CROATIA MARIO MANDUZKIC aliyezaliwa mwaka 1986.
BVB walianza mchezo kwa kasi sana huku beki wa kulia mpoland Lukasz Piszczek akifanya kazi nzuri ya kumtia mfukoni FRANK RIBERY na mwenzie MARCEL SCHMELZER akakaba na kushambulia vizuri sana na kumthibiti ARJEN ROBEN na pengine katika dakika 20 za mwanzo,BVB wangeweza hata kupata goli 2.Dakika 25 za mwisho wa kipindi cha kwanza,BAVARIANS waligeuka baada ya kukoswa magoli kibao na kuanza kurudi mchezoni.Walitengeneza nafasi kadhaa ingawa zote hazikuzaa matunda.
Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika,kipa NEUER na WEIDENFELLER ndo walikuwa mashujaa wa mchezo.wote kwa awamu tofauti,waliweza kuokoa mipira mingi sana langoni mwao.
Kipindi cha pili hakikuwa na mwenyewe JEROME BOATENG beki wa BAVARIANS alionekana kuchoka kidogo na hasa alipochezewa rafu na mpoland Robert Lewandowski,huku Arjen Roben na Frank Ribery wakiruhusiwa kucheza na hapa ndipo BVB walipojichanganya.
Upande wa dimba nadhani inajulikana kwamba BVB magoli yao mengi yanatokea katikati kwa hiyo ni ishara tosha kwamba wao wanaviungo hodari.Schweinstiger na Martinez walipotezwa jana nakina BENDER na pacha wake GUNDOGAN aliyefunga kwa mkwaju wa penati.Penati ilikuwa halali na wakati mwingine DANTE angeweza hata kupewa kadi sema refa aliona adhabu ya penati inatosha.
mwisho wa siku lazima tukubali kwamba,BAVARIANS ndo mabingwa wapya wa ligi ya mabingwa ULAYA na hawakubahatisha.ARJEN ROBEN nadhani Ballon D'or itamuhusu.
Home
»
Unlabelled
»
Share This To :
0 comments:
Post a Comment